SOKO LA FERI LIPO HATARINI KUTOKANA NA UHABA WA VYOO
Soko maarufu la samaki lililopo maeneo ya feri jijini Dar es salaam jirani na Ikulu linatishia hali ya usalama kwa wateja na wavuvi. Suala la usafi wa mazingira limekuwa likipigiwa sana kelele na mpaka baadhi ya wafanyabiashara wengine wamefungiwa biashara zao kutokana na kukithiri kwa uchafu,lakini hali ikoje katika soko la Feri kiafya? .
Tovuti hii ilishuhudia baadhi ya wavuvi na wanaojishughulisha na shughuli za kuvua na kupara samaki katika soko hilo, wakijisaidia haja ndogo (kukojoa) pembezoni mwa bahari huku shughuli za uvuvi na kupara samaki zikiendelea kama kawaida,kana kwamba jambo hilo sio lenye kuhatarisha afya.
Zourhadg ilizungumza na mwenyekiti wa soko la Feri Bwana Rajab R Mng’oi ambaye alikiri kuwepo na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa vyoo katika soko hilo pamoja na gharama ya kulipia huduma hiyo ya choo.
Ameeleza kuwa soko hilo lina jumla ya vyoo 2, vyenye matundu 6, ambavyo havitoshi, huku akiweka wazi kuwa kutokana na wingi wa watu lazima uharibifu wa mazingira utokee.
Aliweka wazi kuwa vyoo hivyo havitoshi kutokana na kuelemewa na wingi wa wafanyabiashara katika soko hilo, kwani wanahudumia watu zaidi ya elfu 30, hadi 40 kwa siku hali inayopelekea kuwepo na uhaba wa huduma hiyo.
Mwenyekiti huyo ameiomba halmashauri juu ya umiliki wa vyoo hivyo kutolewa kwa wakandarasi na kurudishwa kwa wadau wenyewe wanauweza kusaidiana na kusimamiwa na kamati ya wadau wenyewe .
0 comments:
Post a Comment