IMEBAINIKA kuwa wapo baadhi ya
wasanii wa filamu na muziki nchini kuwa na tabia ya kujipiga picha za uchi na
kuzitumia visivyo ikiwemo kuzituma kwenye mitandao hali inayochangia mmomonyoko
wa maadili nchini.
Sakata la kusambaa kwa picha hizo zisizokuwa
na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limeibuka tena
bungeni likiwa na sura mpya huku baadhi ya wabunge wakitaka kujua serikali
inachukua hatua gani juu ya picha zilizosambaa juzi zinazomuonesha mmoja wa
wabunge (jina kapuni) akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alikanusha na kudai
si za kwake.
Moto huo ulizidi kuwaka bungeni leo
katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Mchinga (CCM), Mhe. Said
Mtanda amehioji serikali wamechukua hatua gani dhidi ya vitendo vya uchapaji wa
picha zisizozingatia maadili huku akiwataja Wema na Diamond kupiga picha wakiwa
chumbani na kuweka kwenye mitandao.
Katika majibu yake Naibu waziri
Habari Utamaduni na Michezo Mheshimu Mkamia, alijibu kuwa serikali imebaini juu
ya matumizi hayo ya picha
Mheshimiwa Habib Mnyaa aliuliza
swali la nyongea kwa wizara ya mawasiliano ya sayansi na teknolojia ambapo jibu
hilo lilijibiwa na waziri wa mawasiliano
Katika majibu yake waziri wa
mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema
“Mhe. Spika
kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu
na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa
zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia
juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge
Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa
zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake
na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi
zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake
zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini
zilipotoka.”
0 comments:
Post a Comment