BAADA ya habari kusambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, juu ya
tuhuma za mume wa muimbaji wa nyimbo za Injiri Flora Mbasha, Emmanuel
Mbasha hatimaye jeshi la Polisi limethibisha kupokea tuhuma za ubakaji
dhidi ya mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha anayefahamika kwa jina
la Emmanuel Mbasha.
Akidhibitisha juu ya kutokea kwa tukio hilo,
kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi ameeleza
kuwa jeshi hilo limepokea tuhuma hizo kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni
binti mwenye umri wa miaka 17 na kwamba binti huyo alifika katika kituo
cha polisi akiwa na ndugu zake. “Taarifa zimepokelewa na
zinachunguzwa. Taarifa zilizokuja ni za kubaka sasa tunazichunguza
tufike mwisho tujue ni nini.”alisema Kamanda Minangi
Ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mlalamikaji polisi
walienda nyumbani kwake ambapo hawakumkuta yeye na mkewe na kwamba hadi
sasa hawajapatikana.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment