• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

MOYES ACHUNGUZWA NA POLISI

Aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes anachunguzwa na polisi nchini Uingereza baada ya kushtumiwa kuhusika katika mapigano katika baa moja ya mvinyo iliyoko katika kitongoji cha Lancashire.

Maafisa wa polisi walifahamishwa saa nne usiku saa za Uingereza kuhusu tukio ambalo kijana mmoja mteja katika baa ya Emporium iliyoko Clitheroe alidai kapigwa na mtu ambaye ilibainika kuwa ni kocha huyo aliyefutwa kazi wa Manchester United.

Hakuna aliyekamatwa katika tukio hilo huku polisi wakiendesha uchunguzi wao kuhusu nini kilichochea uhasama baina yao wawili.

Watu kadha walioshuhudia wamekuwa wakidai kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alimgoa kocha Moyes kutokana na matokeo duni ya Manchester United alipokuwa mkufunzi kwa miezi kumi na hivyo kumuudhi sana Moyes aliyemfokea na kumburuta.

Moyes alitimuliwa Old Trafford mapema mwezi huu yapata miezi 10 tangu achukue uskani kutoka kwa kocha mkongwe Sir Alex Fergusson aliyestaafu.

Alikuwa ametokea Everton ambayo alikuwa ameiongoza kwa zaidi ya miaka 10.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment