Baada ya kuzushiwa kufa muigizaji wa Bongo Movies Dr Cheni ameandika ujumbe mfupi kulaani kitendo hicho cha baadhi ya watu kumzushia kifo. Hali hiyo imeibuka mara baada ya msanii huyo kuugua ugonjwa wa homa ya Dengue, zaidi ya wiki moja ingawa hivi sasa yupo katika hali nzuri na ameruhusiwa kutoka hospitali.
“Jaman kifo kipo na hakuna atakaye kwepa ni lazima tutakufa na hakuna atakayebakia ila si vyema kunizushia cku yangu itafika tu na wote mtajuwa lakin si jambo la busara kunizushia.” Dr Cheni Ameandika kwenye Instagram.
Nae Elizabeth ‘Lulu’ Michael alipost picha ya Dr Cheni kwenye instagram na kuandika:
“Jamaani kuna mambo ya kuzushiana lakini sio KIFO,kuna habari zimezushwa kwamba @drchenitz Cheni amefariki....ni habari za uongo jmn....yuko salama kabisa na juzi ameruhusiwa kutoka hospital na anaendelea vzr...Tunajua kufa ni wajibu lkn mpk Mungu mwenyewe apende...!!!!Pole baba angu”
0 comments:
Post a Comment