Maafisa nchini Colombia wanajaribu kuwanusuru takribani watu thelathini waliozikwa wakiwa hai na mamia ya tani ya tope pamoja na mawe baada ya mgodi haramu wa dhahabu kuporomoka usiku wa jumatano.
Miili ya watu 3 imepatikana huku zoezi hilo likionekana kuwa gumu zaidi kutokana na udongo huo kulowa chepechepe katika eneo hilo la tukio.
Waokoaji wanajaribu kufukua udongo ili kuwanusuru watu waliozikwa .Takriban mashine saba za kufukua udongo zimekuwa zikihusika katika shughuli ya uokozi katika mgodi huo ulioko kusini magharibi mwa sehemu ya Cauca linaonekana kuwa gumu.
Kando kando mwa mgodi huo wapo mamia ya jamaa na marafiki ya wachimba migodi waliofukiwa ambao wanafuatilia kwa karibu shughuli za uokoaji.
Lakini mmoja wa wazima moto amesema kuwa hamna matumaini makubwa .Huku matumaiani yakizidi kudidmia , Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos ameulaumu uchimbaji migodi haramu kwa kusababisha vifo hivyo .
Amesema serikali yake inapigana vita dhidi ya uovu huo.Ijumaa wiki iliyopita, wachimba migodi wengine wanne walipoteza maisha yao huku sitini na tano wengine wakiathirika na gesi ya sumu katika sehemu ya Antioquia
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment