• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

SHABIKI ALIYEMTUPIA NDIZI ALVES AKAMATWA

Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya Jumapili akiwa uwanjani. Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati Alves alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili. Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii. Huku ikiwekwa wazi kuwa shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.

Alves amesema kuwa amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi kwa miaka sita .Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.

Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.

Barcelona walishinda Villareal mabao 3-2 katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa El Madrigal mjini Castellon pwani ya Hispania.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment