Waendesha Baiskeli wa Nyanda za Juu Kusini “THE HIGHLANDERS “kushiriki mbio za Muungano Waendesha baiskeli kutoka Mikoa miwili ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na Njombe ambao wanajulikana zaidi kwa jina la “The Highlanders “ wamewasili Dar es saalam kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Baiskeli ya Muungano ya umbali wa Kilometer 118 yakianzia maeneo ya Pugu na kumalizikia Maeneo ya Coco Beach yatakayofanyika Tarehe 19 April 2014.Mikoa iliyothibitisha kushiriki Mashindano hayo ya Muungano ni Arusha ,Dar es salaam, Dodoma, Lindi, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Tanga na kwa upande wa Visiwani Zanzibar
Timu ya “THE HIGHLANDERS” Cycling inawakilishwa na wafuatao
1. Lucas Mikael Mhagama (35 years) Tunduma Momba-MBEYA
2. Jotam Uswege Kimbombo (32 years)kutoka Matema Kyela Mbeya
3. Castrol Abed Msemwa (25 years)Matamba Makete Njombe
4. Ezekiel Laison Msangawale (23 years)Chimala Mbarali Mbeya
5. Biton Henry Lupapa (27 years) Matamba Makete Njombe
6. Elias Zawad Talla (39 years) Mbeya Urban ,Mbeya
Wote mnakaribishwa kuwashangilia waendesha baiskeli hawa!!
0 comments:
Post a Comment