Makamu mwenyekiti wa bunge maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan leo asubuhi amethibitisha kupokea hati ya makubaliano ya muungano ilithibitishwa kisheria.
Katika hatua nyingine wajumbe wa bunge maalum la katiba leo wameendelea na majadiliano kuhusu sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba huku sualoa la Muungano na muundo wa serikali kuzua mjadala mkali.
Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Membe ambaye ni mjumbe wa bunge hilo amesema endapo zitaundwa serikali tatu, ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano, serikali moja ya Muungano itapoteza uthabiti wake.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment