• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

WAPINZANI WASUSA KIKAO CHA BUNGE


Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameondoka kwa hasira katika kikao cha bunge hilo kinachoendelea mjini Dodoma. Hasira yao inatokana na madai kwamba maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya yamekuwa yakipuuzwa.
Wajumbe wa bunge hilo ambao ni kutoka upande wa upinzani chini ya umoja unaojulikana kama UKAWA, yaani Umoja wa Katiba ya Wananchi, wameamua kutoka nje kupinga kile wanachosema ni kupuuzwa kwa makusudi maoni ya wananchi wanaotaka muungano wa muundo wa serikali tatu kama yalivyopendekezwa katika rasimu ya katiba hiyo.
Badhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walio katika Umoja wa UKAWA wameamua kutoka nje wakati wajumbe wakiendelea na majadiliano ya taarifa za kamati ya bunge hilo kuhusu sura ya kwanza na ya sita.

Hatua hiyo imefikiwa na wajumbe hao baada ya kuunga mkono mchango wa Profesa Lipumba ambaye amesikitishwa na jinsi mjadala wa bunge hilo unavyogubikwa na ubaguzi.

Profesa Lipumba amesema wanahitaji katiba itakayo hakikisha kila mwananchi anapata haki yake bila kujali rangi jinsia na makabila msingi alioucha baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Aidha Profesa Lipumba alieza kuwa amesikitishwa na Kauli iliyotolewa na Waziri William Lukuvi wakati wa sherehe ya kumsimika mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu akimwakilisha Waziri Mkuu.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment