Baada ya kubainika kuwa wapo baadhi ya madereva kuendesha magari barabarani huku wakiwa wamelewa, huku wakisababisha ajali, kikosi cha Usalama barabarani kimejipanga kudhibiti madereva wote walevi kwa kuanzisha mchakato mpya wa kuwapima madereva wote hususani wa magari ya safari za mkoani kwa kipimo maalumu kinachojulikana kwa jina la 'Alcohol Tester' au 'Alcoblow'.
Akizungumza na blog hii Zourhadg, Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohammed Mpinga alisema kuwa wameanzisha mchakato huo wa kuwapima baadhi ya madereva wanaoendesha magari ya kwenda mikoani ili kudhibiti madereva waliokuwa na tabia ya kuendesha gari wakiwa wamelewa.
Alisema kuwa zoezi hilo limeanza rasmi jana katika kituo kikuu cha Ubungo huku akisisitiza kuwa ni zoezi la kudumu ambalo litakuwa linafanyika kwa kushtukiza huku likiwa na lengo la kupunguza ajari za barabarani zinazosababishwa na ulevi uliopindukia.
"Tunafikiria zoezi hilo liwe la kudumu na lifanyike Tanzania nzima lakini kutokana na uhaba wa vifaa hivyo hivyo linafanywa kwa uchache na kwa mafungu" alisema Mpinga
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment