WABUNGE WA UPINZANI WACHACHAMA, BUNGE LIMEAHIRISHWA
BUNGE limeahirishwa ghafla leo asubuhi kufuatia wabunge wa Upinzani kusimama na kukataa kutoka nje ili kuzuia Miswaada mitatu ya Gesi Petroli na uzinduaji kusomwa kwa hati ya dharura.
Wabunge hao wa upinzania wanataka miswaada hiyo ijadiliwe kwanza na wadau kabla haijasomwa bungeni hapo.
Hali iliyopelekea SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda, kulazimika kuairisha bunge lililokuwa likiendelea mjini Dodoma leo asubuhi mara baada ya kutokea hali ya sintofahamu kwa baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani kwa kile kinachodaiwa kuwasilishwa kwa miswaada mitatu kwa hati ya dharula.
Ambapo mbunge wa kambi ya upinzani John Mnyika aliomba muongozo kwa spika juu ya kile kinachodaiwa kukiukwa kwa kanuni zilizopangwa kwa kuwasilishwa mswaada wa sheria kwa hati ya dharula, mswaada wa sheria ya petrol wa 2015, mswaada wa sheria ya usimamizi wa mapato mafuta na gesi ya mwaka 2015, Mswaada wa sheria uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment