Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mh Paul Makonda amewataka watanzania kutokubali kumchagua Rais mla rushwa na fisadi hata kama atapitishwa na chama chake cha CCM.
Akizungumza na ripota wa Timesfm.co.tz, Makonda amedai yeye hatokubali kulishuhudia swala hilo kwa sababu kama rais hatakuwa muadilifu , hata mawaziri na serikali yake kwa ujumla hawatakuwa na utu heshima na maadili kwa jamii.
“Tena naomba niliseme hili, watanzania wenzangu na wana Kinondoni tusikubali kuchagua Rais mwizi hata kama atatoka ndani ya CCM, jitu jizi, mla rushwa, alafu bado tumshangilie hii haipo sawa
Siku rais Kikwete anakabidhi madaraka pale uwanja wa taifa, eti anamkabidhi rais mwizi ndio siku na mimi napeleka barua moja kwa moja ya kuacha kazi kwa sababu nataka kuingia mbinguni” alisema Makonda.
Kwenye “line” nyingine Paul amebainisha mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya wilaya ya Kinondoni ndani ya siku 100 tangu aingie kazini, kuwa ni kupambana na kutatua Migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment