Times fm kupitia kipindi cha “The jump off”, wameandaa shindano na tamasha kubwa la kuinua vipaji vya wasanii wa hip hop lililopewa jina la “JUMP OFF MICHANO”
Akizungumza na tovuti ya Timesfm.co.tz mratibu wa shindano hilo mtangazaji Jabir Saleh, amesema wasanii wengi wa hip hop wamejitokeza kuungana na watanzania siku hiyo katika kutafuta vipaji vipya vya muziki nchini.
Jabir amewataja baadhi yao kuwa ni Rapper Zaid, Nash mc, Songa, Inspector Haroun, Wakazi na P the mc.
“mi nawasihi tu vijana wajitokeze kwa wingi kwa kuwa tumeandaa zawadi pamoja na kuwaendeleza kimuziki kupitia Times fm, kutakuwa na rappers wakali pia kwa ajili ya burudani” amesema mtangazaji huyo.
Kinyang’anyiro hicho kitafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Madenge Temeke, jumamosi hii ya tarehe 13 mwezi wa 6 ambapo mshindi atarekodi nyimbo chini ya producer wa B hits “Hermy b” na Josbless pamoja na mkwanja wa laki 5.
SOURCE: TIMESFM
Home / Entertainment
/ WANAMUZIKI NASH MC, SONGA, WAKAZI , INSPECTOR HAROUN NA P THE MC KUKINUKISHA JUMP OFF MICHANO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment