• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

WALIMU 100 WASIMAMISHWA KAZI KWA KOSA LA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

KAMATI ya tume ya huduma ya walimu nchini Kenya, imewafungia zaidi ya walimu mia moja baada ya kukumbwa na makosa mbalimbali ikiwemo ya udhalilishaji wa kijinsia.

Ambapo  kamati hiyo imesema imekuwa ikiwachunguza walimu hao na kuwabaini makosa mbalimbali ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia, hali hiyo iliwapelekea walimu hao kuondolewa  usajili rasmi wa walimu na hawatoruhusiwa kurejea kufundisha nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Kenya  Tume ya huduma ya walimu imetoa majina ya walimu wote 126 ambao wamesimamishwa kazi kwa madai ya tabia chafu.

Taarifa inasema kuwa walimu hao walifukuzwa kazi baada kupitia mchakato wa kinidhamu ambao umewakuta na hatia ya makosa mbalimbali.

Walimu wawili waliofutwa kazi ni wanawake.Taarifa hiyo ilionya kwamba, kama mwalimu yeyote kati ya waliofungiwa atadharau uamuzi huo, basi atapigwa faini ya  dola za Kimarekani 50 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la idadi ya walimu ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa tabia chafu huku baadhi yao wakihusika kuwadhalilisha wanafunzi kijinsia.

Walimu kadhaa wamekuwa wakifikishwa mahakamani na wengine kusimamishwa kazi. Mwezi April 2013, mwalimu wa sekondari huko Magharibi mwa Kenya alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19. Mwalimu huyo aliachiwa kwa dhamana na ni miongoni mwa wale waliofungiwa na tume ya huduma ya walimu.

Mwanzoni mwa wiki hii mwalimu mkuu huko Nyaza alikamatwa na polisi baada kumvua nguo mwanafunzi wa kike kwa sababu alivaa sketi fupi. Mwalimu huyo anaendelea kushukiliwa na poliosi.Mara nyingi kesi zimekuwa haziishi ambapo kwa kiasi kubwa hushughulikiwa na TSC mamlaka za shule. Wakati mwingine tatizo hili limekuwa likishughulikiwa kati ya wazazi na walimu.

Afisa wa shirika linalosimamia ustawi wa watoto nchini Kenya ambaye hakutaka jina lake litajwe, amemtaka mwendesha mashtaka wa serikali kuzichukua kesi na kuhakikisha watuhumiwa wa ngono dhidi ya watoto wadogo na wanafunzi wanapawsa kufikishwa mahakamani.

Nao Umoja wa walimu wa shule za msingi nchini Kenya umeelezea msimamo wake kwamba hawatomlinda mwanachama yeyote atakayekiuka maadili. Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Kenya Musau Ndunda ameitaka tume ya walimu kuwachunguza walimu wote ili kuzuia watoto wadogo kudhalilishwa kijinsia.

USIKOSE KUSIKILIZA MASKANI YA 100.5TIMESFM KILA SIKU SAA 10JIONI HADI 1KAMILI KUPATA UNDANI WA SAKATA HILI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment