• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

SURA YA MWANAMKE KUONEKANA KATIKA NOTI YA DOLA KUMI

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja, noti mpya ya dola kumi nchini Marekani itakuwa na picha na mwanamke.

Wizara ya Fedha ya Marekani imewataka wananchi wa Marekani kutoa mawazo yao ni picha ya mwanamke gani ichapishwe kwenye noti hiyo.

Wizara hiyo imesema inatafuta kile kinachoelezwa kuwa demokrasia shirikishi.

Kwa sasa noti za Benki Kuu ya Marekani zilizo katika mzunguko wa fedha zinawaonyesha viongozi wa zamani wa kisiasa----wote wakiwa wazungu.

Noti hiyo mpya ya dola kumi itatolewa mwaka 2020 kuadhimisha miaka mia moja ya wanawake wa Marekani kupata haki ya kupiga kura.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment