• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

LOWASSA, MEMBE WASHAURIWA KUJITOA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS ILI KUNUSURU CHAMA




IMESHAURIWA kuwa Mh. Edward Lowassa na Bernard Membe kujitoa katika kinyang’anyiro cha Urais ili kukinusuru chama cha Mapinduzi (CCM) kisisambaratike kutokana na nguvu ya makundi yaliyojengwa ndani ya chama hicho kupitia majina yao.

Ambapo imebainika kuwa wawili hao ambao wameshatangaza nia ya kuomba ridhaa ndani ya chama chao kuchaguliwa ili kuwania urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wajitoe kwenye kinya’nganyiro hicho ili kukinusuru chama hicho kama wanamapenzi mema na chama.

Hayo yalibainishwa na mwanaharakati Humphrey Polepole alipokua akizungumzia vigezo na uwepo wa watangaza nia ndani ya chama kimoja, ambapo aliweka wazi kuwa Mh. Lowassa na Bernard Membe hao ndio wamepata umaarufu mkubwa katika kinyang’anyiro hicho ndani na nje ya chama na ndani ya chama hali iliyopelekea wanachama wengi kugawanyika.

Wananchama wengi wameonekana kugawanyika wapo walio upande wa Membe, na wengine upande wa Lowassa hali iliyopelekea wawili hao kutokuwa pamoja huku kila mmoja akipiga hatua kubwa mbele na kundi kubwa la watu.

“Siyo siri kwenye CCM ukizungumzia umaarufu hao ndio vinara ingawa bado kwenye chama hawajakubaliana, si ndani ya chama hata nje ya chama wanachama wengi wanaonekana kugawanyika kwa upande wa Membe na Lowassa na hawa watu hawakabiliani, kila mmoja akipiga hatua kubwa kwenda mbali” alisema Humphrey Polepole.

Ambapo alifafanua kuwa Membe na Lowassa wanaonekana ni watu waliokuwa na makundi makubwa ndani ya chama, huku akitolea mfano wa makundi hayo yalishawahi kutokea mwaka 1995 na 2005 hali inayopelekea kukiweka chama katika sehemu mbaya.

Aliweka wazi kuwa kutokana na hali hiyo maamuzi ya busara yanatakiwa kutumika ili kukinusuru chama hicho, huku akifafanua zaidi kuwa wawili hao wanaweza kuwa msingi wa kukivuruga chama cha Mapinduzi.

“Hawa wawili wasipokaa wazee, watu wazima wenye busara na vijana wanaojitambua kwenye chama cha mapinduzi kuona ni namna gani hawa wawili kampeni zao haziendi mbele zaidi ya maslahi mapana ya kuimarika na kubaki kitu kimoja chama cha mapinduzi, wanaweza kuwa msingi wa kukivuruga chama cha mapinduzi, wanaweza kuwa na dhamira njema ya kuwa Rais lakini harakati zao za kuutafuta urasi huu zinaweza kugharimu chama cha mapinduzi, uamuzi usiokuwa raisi ambao mimi naweza kuushauri hawa wawili chama kiwaweke pembeni kwa maslahi ya chama, ni maamuzi magumu kabisa”. Alisema Polepole.

Alisema kuwa wawili hao namna wanavyoendesha kampeni zao kila mmoja anakundi kubwa la watu huku wakionekana kutumia matumizi makubwa ya fedha .
Je unataka kujua Mwigulu Nchemba, January Makamba wao wameshauriwa nini?, je Samweli Sitta na Wassira unataka kujua wameambiwa nini jiunge na Maskani ya 100.5 timesfm leo kuanzia saa kumi jioni hadi moja kamili kupata story kamili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment