NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Mh. Charles Mwijage ameagiza kampuni yakuuza mafuta nchini kuendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi kwa kuwa serikali inayo hifadhi kubwa ya mafuta.
Naibu Waziri ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na uwepo wa mgomo katika siku zinazokuja kutokana na kuwepo kwa uhaba wa mafuta ya Petroli na diseli na kusema kuwa serikali itawachukulia hatua wamiliki wa kampuni ya mafuta pale watakapobainika kukiuka na kuvunja sheria.
"Ni kweli na mimi nimeona kwenye mitandao ya kijamii taarifa inayoonesha kukosekana mafuta kwa siku hizi mbili, lakini haiwezi kutokea kwa sababu tunajua kwa takwimu kwamba kwenye hifadhi ya Dar es Salaam, tuna mafuta ya kutosha" alisema
Alisisitiza kuwa wamiliki wa kampuni zinazotoa huduma ya mafuta wasijalibu kuzuia uuzwaji wa mafuta kwani sheria za EURA zinaweza kumfungia mtu yoyote anayezuia mafuta kuuzwa, huku akiweka wazi kuwa leseni ya uuzwaji wa mafuta ni mali ya waziri hivyo wanaweza kuchukua leseni muda wowote kwa yeyote anayekiuka sheria za uuzaji wa mafuta.
0 comments:
Post a Comment