Tamasha kubwa la wazi la watoto lililozinduliwa rasmi mwezi March, litafanyika May 31, 2014 katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam. Tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili, May 31 na June Mosi mwaka huu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Waandaaji wa tamasha hilo wamesema watu ambao wangependa kuwa na vibanda vya maonesho ya bidhaa au huduma za watoto/ familia wafanye booking muda huu kupitia namba 0767 897 au 0713 673 222 au barua pepe kidsfesttz@gmail.com.
Meneja masoko wa Extreme Kids Events, Yvonne Moyo amesema katika tamasha hilo kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya watoto, elimu kwa familia nzima kupitia semina pamoja na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya watoto.
Katika tamasha hilo, watoto wataingia kwa shilingi 3,000/- na wakubwa watalipa shilingi 5,000.
Tamasha hilo ni endelevu na mwaka huu litafanyika katika mikoa mitatu, baada ya Dar es Salaam litafanyika Arusha October 4 hadi October 5, Mt. Meru Hotel Gardens. Mwanza litafanyika December 6 hadi December 7, katika uwanja wa Nyamagana.
“Extreme Kids Festival ni tukio kwa ajili ya familia nzima. Sababu ya kusema ‘Extreme’, ni kwa kwa kuwa tunataka wazazi, watoto wote na yote yanayohusu afya, madaktari, wote wanaohusika na elimu hata midoli…kuwa pamoja katika tukio moja na kisha tunaweza kuwa na muziki na tamasha la familia. Hakutakuwa na pombe kabisa, na hii ni kwa ajili ya kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya watoto na familia.” Alisema Yvonne Moyo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment