VITENDO VYA ULAWITI NA UBAKAJI VIMEONGEZEKA NCHINI
Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania (LHRC), imebaini kuwa watoto 863 kulawitiwa na 10 kubakwa na wazazi wao au ndugu wa karibu nchini Tanzania kwa mawaka 2013,huku mkoa wa Dar es Salaam, Arusha pamoja na mwanza kukithiri kwa vitendo.
Ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Shirika hilo inaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini huku kumi kati yao ikionesha kufanyiwa ukatili na wazazi wao wenyewe.
Ripoti hiyo ya haki za binadamu kwa mwaka 2013 ilitolewa jijini Dar es Salaam imebainisha hayo kutokana na utafiti uliofanywa na Kituo hicho cha sheria na Haki za binadamu -LHRC kwa pamoja na kituo cha huduma za sheria Zanzibar.
Akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba, amesema watoto wamekuwa katika maisha ya hatari Zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya ubakaji.
Huku akiweka wazi kuwa ripoti hiyo imebainisha mkoa wa Dar es Salaam, Mwanza pamoja na Arusha kuwa na ongezeko kubwa la kutokea kwa vitendo hivyo .
Ambapo amebainisha kuwa ongezeko la vitendo hivyo nchini vinatokana na kushindikana kuchukuliwa hatua pindi matukio hayo yanapotokea hali inayopelekea baadhi ya wananchi kuendelea kufanya vitendo hivyo.
Aidha vitendo vya kishirikina imeonekana ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kuwepo na tatizo hilo nchini huku baadhi ya wazazi wakiamini pindi wanapofanya vitendo hivyo vya ulawiti vinapelekea kupata utajili.
Ripoti hiyo ambayo ni ya 11 kutolewa na taasisi hiyo imebainisha kuwepo kwa matukio ya raia kuwaua raia wenzao ambayo yameongeza kasi za ukiukwaji wa haki za kuishi nchini humo.
Aidha utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya 1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira kali katika matukio tofauti, huku askari polisi nao waliwaua raia 28 katika kipindi cha mwaka 2013.

0 comments:
Post a Comment