JESHI la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia msichana mwenye umri wa miaka 19, Husna Iddi Kisoma, mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za mauaji ya mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa kimapenzi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei, aliweka wazi kuwa, tukio hilo lilitokea juzi usiku huku ikidaiwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu mwanamke huyo kujihusisha kimapenzi na wanaume wengine.
Akizungumza na tovuti hii kamanda Matei, alisema kuwa tukio hilo lilitolea juzi eneo la Mkuranga ambapo ugomvi huo ulikuwa mkubwa hali iliyopelekea mwanamke huyo kushika sehemu za siri za mwanaume huyo na kumvuta hali iliyopelekea kusababisha kifo cha mwanaume huyo.
Aliweka wazi kuwa baada ya tukio hilo mwanaume huyo alipata maumivu makali ambapo alikimbizwa hospitali ya Mkulanga lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya hali iliyosababisha umauti wake.
Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo teyari ameshafikishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment