• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

MWANAFUNZI AJIUA AKIJARIBU KUJITOA MIMBA

IMESIBITISHWA kuwa mwanafunzi mmoja wa chuo cha Eden Hilling College aliyefahamika kwa jina la Atu Gabriel amefariki akiwa yupo katika chumba cha mpenzi wake mara baada ya kujaribu kutoa mimba kwa njia ya vidonge.



Akizungumza na tovuti hii kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa katika chumba cha mwanaume huyo anayesemekana kuwa alikuwa ni mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Hafidhi.

Kamanda Ulrich ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa marehemu ukiwa karibu na vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi na kwamba polisi wanaendelea kumtafuta bwana Hafidhi ambaye alidaiwa kukimbia baada ya tukio.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali Kamanda huyo aliweka wazi kuwa mwili wa marehemu huyo ulibainika kuwa alikuwa na ujauzito na alikuwa akijitahidi kutoa ujauzito huo kwa kutumia vidonge
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment