• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

ABIRIA 160, WAOKOLEWA KATIKA MELI ILIYOZAMA PWANI YA KOREA KUSINI


Imeripotiwa kuwa meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika Pwani ya Korea Kusini imekumbwa na dhoruba ambapo teyari shughuri za uokoaji zinaendelea.

Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli hiyo, ilioyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini. Ambapo maafisa  wameeleza  kuwa walinzi wa pwani hiyo, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji , zimepelekwa katika ferry moja inayozama kusini mwa pwani hiyo.


Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi, Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea. Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .

Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe. Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kusakama maji zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea huku duru zikidhibitisha kuwa mtu mmoja amepatikana ameaga dunia.

SOURCE : BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment