WATU 35 WAMEPOTEZA MAISHA KWA UNYWAJI WA POMBE
HII KALI: WATU 35 wamepoteza maisha na wengine kulazwa kwa unywaji uliokithiri wa pombe haramu aina ya Gongo katika mji wa Mumbai nchini India.
Waziri kiongozi wa jimbo la Maharashtra ametoa agizo la kufanyika uchunguzi, kwa baadhi ya watu waliokamatwa kwa unywaji wa pombe hiyo haramu.
Pombe haramu aina ya gongo inayotokana na mahindi inanyweka kwa kiasi kikubwa nchini kote India ambako wakati mwingine pombe hiyo inauzwa chini ya dola moja ya Kimarekani, ikisababisha vifo vya mara kwa mara.
Karibu watu 170 wameripotiwa kufa katika jimbo la Bengal baada ya kunywa pombe hiyo maarufu kama "moonshine"

0 comments:
Post a Comment