• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

TALAKA ZAWATESA WATOTO

Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Zainab Omar Mohammed amesema wimbi la ndoa kuvunjika visiwani hapa limekuwa likisababisha familia nyingi kuishi katika mazingira magumu.

Waziri Mohammed alisema hayo alipofunga mjadala wa makadirio na matumizi ya bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2015/2016 katika kikao cha bajeti kilichofanyika Chukwani, Zanzibar.

Alisema ndoa zinapovunjika watoto wanakosa haki zao za msingi ikiwamo elimu, huku wanawake wakiishi katika mazingira magumu.

Waziri Mohammed alitaja sababu za ndoa hizo kuvunjika kuwa ni migororo ya wanandoa, udhalilishaji, kukosa uaminifu na watoto kutopewa matunzo.

Hata hivyo, alisema wizara inalifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na viongozi wa dini na jamii ili kupungua matatizo hayo.

Alisema kwamba kesi nyingi za udhalilishaji wanawake na watoto zinashindwa kupata mwelekeo mzuri katika Vyombo vya sheria kutokana na tatizo la kupatikana kwa ushahidi wa kutosha pamoja na kesi zenyewe kuharishwa mara kwa mara na kuwakatisha tamaa wahusika.

Awali, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Makame Mshimba Mbarouk, Hamza Hassan Juma, Viwe Khamis Abdalla na Wanu Hafidh Ameir walitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kusimamia kesi za unyanyasaji wanawake na watoto.

Hata hivyo, Waziri Mohammed alisema suala hilo linahitaji ushirikiano na mamlaka mbalimbali zinazosimamia sheria.

Pia alisema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano wakati wa upelelezi wa kesi husika ikiwamo kutoa ushahidi mahakamani.

Alisema wizara yake imekuwa ikifuatilia kesi za udhalilishaji lakini bado hali ni ngumu na inakatisha tamaa kutokana na kesi nyingi kuvurugwa na kuchukua muda mrefu kusikilizwa, huku uamuzi wake ukiwa hauridhishi.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inaendelea na mpango wake wa kununua mashine ya kuchunguza vinasaba (DNA) ili kukusanya vielelezo hasa katika kesi za ubakaji pamoja na makosa mengine ya jinai.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment