• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

BAADA YA KUFUNGA NDOA YA JINSIA MOJA ANYIMWA LESENI



HII imetokea hivi karibuni, Kasisi mmoja ambaye amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kunyimwa leseni ya kufanya kazi kama muhudumu katika zahanati ya afya kwa kuwa amefunga ndoa ya jinsia moja.

Hali hiyo imepelekea mkaka huyo kushitaki kanisa kwa kumbagua kutokana na hali yake hiyo ya kufunga ndoa ya jinsia moja na kudai kuwa anahaki ya kufanya chochote kama walivyo watu wengine.

Kasisi Jeremy Pemberton alikuwa amewasilisha pendekezo la kutaka kuhudumu kama Kasisi katika kanisa lililoko ndani ya hospitali.

Aidha kasisi Pemberton anadai kuwa maombi yake yalipingwa kwa kinywa kipana na kaimu askofu wa Southwell na Nottingham nchini Uingereza.

Rt Revd Richard Inwood alimkashifu kasisi Pemberton kuwa katika ndoa na mwanaume mwenza ambaye ni kinyume na mafundisho ya kanisa la Church of England.

Tume inayosimamia utoaji kazi nchini Uingereza inatazamia kuanza kuisikiza kesi hiyo leo.

Wadau wa maswala ya ajira wanasema kesi hiyo inatumiwa kama funzo na mtihani kwa tume hiyo ya ajira ya uingereza iwapo itazingatia haki za wafanyikazi ama zile za mwajiri.

Kasisi Pemberton alikuwa mhudumu wa kwanza kanisani kuoa nchini Uingereza.

Pemberton alifunga pingu za maisha mnamo mwezi wa Aprili mwaka wa 2014.

Askofu Inwood, alimnyima kazi kasisi Pemberton, na kisha akaiandikia barua bodi inayosimamia hospitali hiyo ya Sherwood Forest akiwashauri wasimpe kazi kasisi Pemberton.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment