• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

AVULIWA TAJI LA UREMBO KISA PICHA ZA UCHI


HII sasa si kitu kigeni kusikia mshindi wa urembo kuvuliwa taji kutokana na sababu mbalimbali, ilitokea Tanzania katika  mitandaoni na Magazetini, watu wakiipigia chapuo  ishu ya Umri, Elimu, na mengine mengi yanayomhusu aliyekuwa Miss TZ, Sitti Mtevu, hali iliyopeleka mrembo huyo kuvua Taji hilo ili kupisha kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

Hii nyingine nayo imetokea nchini Zimbwabwe kwa aliyekuwa mrembo nchini huyo aliyeshinda taji hilo mwaka 2015, Emily Kachote kuvuliwa taji hilo baada ya kuzaaga kwa picha zake za utupu.

Kwa mara ya pili mfululizo waandaaji wa shindano la malkia wa urembo nchini Zimbabwe wametupilia mbali ushindi wa taji hilo uliomwendea malkia wa urembo kufuatia sakata la picha za uchi.

Emily Kachote alikuwa ameshinda taji la malkia wa urembo nchini Zimbabwe mnamo mwezi Aprili na alitarajiwa kuwakilisha taifa hilo katika mashindano ya dunia ya malkia wa urembo nchini Uchina mnamo mwezi disemba.

Lakini waandalizi wa taji hilo wanasema kuwa bi kachote alikiuka sheria ya shindano hilo ambalo linapinga wanaoshindana kupiga picha za uchi .


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment