• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

ANGALIA VIDEO YA NANA, NA NITAMPATA WAPI YA DIAMOND PLATNUM

Hongera sana msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum kwa kazi nzuri ya muziki ambayo inapelekea kupeperusha bendera yetu ya Taifa ndani na nje ya nchi kwa kazi nzuri unayoifanya.

Umeweza kubadilisha upepo wa sanaa nchini huku ile kadhia ya kudhurumiwa na kufanya shoo za bei rahisi ikiwa inapotea miongoni mwa mapromota, na kuufungua ukurasa wa kuufanya muziki kuwa biashara.

Hatua kubwa umepiga kwa kuendelea kunyakua tuzo mbalimbali nje ya Tanzania hiyo pia inaashiria juhudi na uwezo wa kufanya jambo kwa umakini na malengo zaidi, pengine umekuwa mwalimu kwa baadhi ya wasanii sasa nao wameamka kuwekeza katika utengenezaji wa video hadi hatua ya wao kwenda kufanya video za muziki nje.

Ingawa kwangu hilo si jambo kubwa sana la kuupima muziki, ila umeleta changamoto kubwa kwa waandaaji wa video wa hapa nyumbani kuwa wabunifu ili kukabiliana na changamoto zinazowafanya baadhi ya wasanii akiwemo Diamond kukimbilia nje ya nchi kufanya muziki.

Nikizungumzia video ya "Nana" ambayo msanii huyo ameitoa hivi karibuni huku ikionekana kufanya vizuri katika mitandao ya kijamii, kwa upande wangu ni video nzuri iliyojaa ubunifu, ingawa nilipoanza kuiangalia ilinijia taswira ya video ya wimbo wake unaoitwa "Nitampata wapi". Kuna vitu ambavyo Diamond anaonesha tofauti kila video anayoifanya hii inaonesha anakuwa kila siku kimuziki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment