• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

PAPA FRANCIS AOMBA RADHI WATOTO KUDHALILISHWA KINGONO

Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameomba msamaha kwa niaba ya watoto waliofanyiwa vitendo vya ngono ambavyo vimepelekea kuchafua kanisa hilo.

Ijumaa  iliyopita Papa Francis alikaririwa akisema anajisikia kuwajibika kwa vitendo vya kingono walichofanyiwa watoto ambavyo vimelichafua kanisa katoliki, na hivyo kuomba radhi. Papa alitoa tamko hilo alipokutana na NGO (taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusha na watoto wakikatoliki) International Catholic Child Bereu (BICE).

“Binafsi nawajibika kuchukua dhambi zote zilizofanywa na wachungaji, ni wachache kwa kuwahesabu, ukifananisha na idadi ya wachungaji, ili niombe msamaha kwa uharibifu waliofanya kwa kuwadhalilisha kingono watoto.

Kanisa linaelewa kuhusu uharibifu huo, ni binafsi, uharibifu wa maadili uliofanywa na wanaume wa kanisa, na hatutapiga hatua hata moja kurudi nyuma na kujutia kuhusu tunavyolishughulikia tatizo hili, pamoja na adhabu zinazostahili kuchukuliwa” Papa aliongeza

Papa Francis alisistiza kuwa watoto ni lazima walindwe dhidi ya nia zote mbaya, ikiwa ni pamoja na utumikishwaji, kuingizwa jeshini, na “kuwapa haki ya kukua katika familia yenye baba na mama”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment