MWANAUME AUWAWA AKIDHANIWA MUUZA DAWA ZA KULEVYA
Kumeibuka na vurugu kubwa kati ya jeshi la polisi pamoja na wananchi wenye hasira jana usiku katika maeneo ya mji mkuu Rio de Janeiro.
Hali ilivyokuwa ni pamoja na barabara zikiwa zimefungwa mjini humo huku risasi zikisikika kutoka eneo hilo huku polisi wakijitahidi kuwadhibiti wakaazi hao.
Ghasia hizo zilitokana baada ya kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 26, Douglas Rafael da Silva, ambaye ni mchezaji densi wa kulipwa.
Kulingana na familia yake mwili wake ulionekana ukiwa umejaa vidonda na walitupia lawama kwa maafisa wa polisi kutokana na kitendo cha kumpiga ndugu yao huyo hadi kufa baada ya kumshuku kuwa anajihusishha na watu wenye biashara ya kuuza dawa za kulevya.
Baadhi ya watu walionekana wakikusanyika katika mklango wa kuingilia katika maeneo ya vibanda hivyo alipoonekana mwili wa kijana huyo akiwa ameuwawa hali iliyopelekea ndugu wa mtu huyo kutaka kujua kwa maafisa wa polisi sababu za kuuliwa kwake.
Polisi kadhaa wa kijeshi wenye silaha wameonekana maeneo hayo baada ya kuzagaa kwa habari juu ya kituo cha polisi kilichoko mahali hapo kuvamiwa.
Pavaozinho ni mojawapo ya makaazi ya mabanda ambayo Serikali Kuu ya Brazil imejaribu kuwatimua magenge ya walangunzi wa madawa ya kulevya wenye silaha kutoka kwa jamii na kueneza amani na mmalaka ya polisi.
Polisi wamekiri katika mahojiano na BBC kuwa wameshindwa kuthibiti usalama katika makaazi ya mabanda katika mji mkuu wa Rio de Jenairo, muda mfupi tu wakati ambapo wageni wengi wanatarajiwa nchini humo, kukiwemo maelfu wanaotarajiwa nchini kwa sababu ya Kombe la Dunia.

0 comments:
Post a Comment