• International News.
  • Fashion News
  • Sports News

MAFURIKO BARABARA ZAFUNGWA, WAKAZI WAZUILIWA KUTOKA NJE YA JIJI LA DAR



Eneo lililokuwa likitumika kuhifadhi mabomba ya kusafirisha gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo hayo ni baadhi ya malori yaliyokuwa yakisafirisha mambo hayo kama picha inavyoonesha magari hayo yamekwamwa kwenye maji .
 Ni geti la kuingilia katika eneo hilo pamoja na ofisi ndogo nyuma ya geti hilo kama eneo hilo linavyoonekana baada ya mvua kubwa kunyesha
Mtu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja bila kujali usalama wake, akijaribu kuogelea ili kwend kuokoa tanki la maji (SIMTANK) lililozolewa na maji, hata hivyo mtu huyo hakufanikiwa kwani maji yalikuwa na kasi kubwa (Picha ndogo) akijitahidi kupambana na maji

IMESIBITISHWA kuwa miondombinu ya jiji la Dar es Salaam imeathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Tanzania nzima huku huduma ya usafiri ikisimama kwa muda hadi hali ya miundo mbinu hiyo kutengemaa.

Hayo yalithibitishwa na Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga, ambapo anaeleza kuwa miundo mbinu ya jiji la Dar es Salaam imeathirika zaidi kutokana kwamba nji eneo la magari mengi kuingia na kutoka

Akizungumza na tovuti ya Zourhadblog, Mpinga aliweka wazi kuwa mvua hiyo imeathiri baadhi ya madaraja ikiwemo daraja la Ruvu lililopo barabara ya Morogoro hali iliyopelekea barabara hiyo kufungwa kwa muda hadi hapo miundo mbinu itakapokamilika.

Hali hiyo imeibua msongamano mkubwa wa magari na kusababisha safari za wasafiri kukwama kutokana na ubovu wa barabara hiyo iliyosababishwa na mvua inayonyesha.

Wakati huo huo Mpinga anaeleza kuwa wamezuia magari yanayotoka kituo kikuu cha ubungo, yanayopitia barabara hiyo ya Morogoro kwenda mikoani ili kuepusha msongamano wa magari wakati barabara hiyo ikiwa katika matengenezo.

Mpinga ameweka wazi  kuwa barabara ya Kilwa pia imeathirika ambapo daraja lilopo katika  mto Mzinga limekatika hali iliyopelekea pia barabara hiyo kufungwa.

Kutokana na tatizo hilo hali ya usafiri  katika jiji la Dar es Salaam leo imekuwa na msongamano mkubwa kutokana na kufungwa kwa barabara Morogoro kutokana na daraja lilopo maeneo hayo kuathirika vibaya.

Pamoja na hayo Kamanda Mpinga ametoa wito kwa wananchi ambao hawana sababu ya lazima kusafiri kwa kipindi hicho wasitishe safari zao hadi hapo hali ya mvua itakapotulia na barabara zitakapomalizika kutengenezwa ingawa kwa sasa hivi juhudi zinaendelea kufanyika.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment